Azam Fc Yaipasua Vibaya Mashujaa

Klabu ya Azam Fc imefanikiwa kutoa kichapo kikubwa kwa klabu ya Mashujaa ya mkoani Kigoma leo baada ya kushinda kwa jumla ya mabao matatu kwa bila katika mchezo wa ligi kuu ya NBC.

Azam Fc baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo katika ligi kuu ya NBC hatimae wamefanikiwa kupata matokeo ya ushindi dhidi ya klabu ya Mashujaa katika dimba la Lake Tanganyika mkoani Kigoma.azam fcMashujaa Fc moja ya timu ngumu sana kufungika msimu huu haswa kwenye uwanja wao wa nyumbani Lake Tanganyika ila leo wamepoteza mchezo nyumbani dhidi ya Matajiri wa jiji la Dar-es-salaam.

Mabao ya wanalambalamba ambayo yamepelekea klabu hiyo kuondoka na alama tatu muhimu leo yalifungwa na Kipre Junior, Djibril Sillah, na mshmbuliaji Allesane Diao ikiwaacha Mashujaa wakiwa hawamini kilichotokea.azam fcKlabu ya Azam Fc wameonekana kurekebisha makosa yao kwa kiwango kikubwa katika mchezo leo dhidi ya Mashujaa tofauti na michezo iliyopita dhidi ya Yanga na Namungo nan ndio sababu ya kuondoka na matokeo chanya katika mchezo wa leo.

Acha ujumbe