Ligi kuu ya NBC hapo jana ilimaliziwa kwa mchezo uliowakutanisha kati ya Azam FC dhidi ya Namungo majira ya saa 2:30 usiku katika dimba la Chamazi.
Azam FC wamepoteza kwa jumla ya mabao 3-1 ikiwa ni mechi ya pili mfululizo wanapoteza kwa jumla ya mabao 6 baada ya kupoteza dhidi ya Yanga wakiwa ugenini siku ya Jumatatu.
Aviator, poker, Roullette, Wild Icy Fruits, Piggy Party na mingine kibao upige pesa na Meridianbet. Ingia www. meridianbet.co.tz.
Namungo wanapata ushindi wao wa kwanza wa ligi kuu baada ya mechi zake sita na jana ilikuwa ya saba ndipo kapata ushindi.
Mabao hayo ya ushindi ya Wauaji wa Kusini yalifungwa na Pius Buswita, Hasheem Manyanya, na Lusajo huku kwa Upande wa Wanalambalamba likifungwa na Lyanga.
Baada ya uhsindi huo Namungo wanasogea hadi nafasi ya 12 ya msimamo wakiwa na pointi sita wakiwa sawa na aliyepo nafasi ya 13 na 14.
Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.
Kwahiyo Matajiri hao wa Chamazi wamesalia katika nafasi yao ya tatu wakiwa na pointi zao 13 baada ya kucheza michezo yao 7.