Klabu ya Azam Fc imetoa taarifa kwa umma na kuweka wazi kua kuna vilabu viwili vimetuma ofa ya kumtaka mchezaji wake Prince Dude ambaye ameomba kuondoka klabuni hapo.
Taarifa ya Azam Fc imeeleza kua imepokea ofa ya vilabu viwili ambavyo ni Al Hilal ya Sudan, Huku taarifa isiyotarajiwa ni kua klabu ya Simba nayo imetuma ofa ya kuhitaji huduma ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Zimbabwe.Matajiri hao wa jiji la Dar-es-salaam wameeleza wako kwenye tathamini ya kutambua ni ofa ipi inafaa zaidi ili waweze kumuuza mchezaji huyo ambaye ameonesha nia ya dhati ya kutaka kuondoka klabuni hapo.
Mabingwa hao wa ligi kuu mwaka 2014 wamesema wanakaribisha vilabu vingine kupeleka ofa klabuni hapo kwa wanaohitaji huduma ya mshambuliaji huyo, Kwani Azam Fc wamesisitiza milango bado ipo wazi.Taarifa iliyoshangaza wengi ni kuona klabu ya Simba kua ni moja ya timu zilizotuma ofa ya kumhitaji Dube, Kwani watani zao klabu ya Yanga ndio ilielezwa mwanzo kua wanamuwinda mchezaji huyo lakini mpaka sasa ni wekundu wa msimbazi Simba waliotuma ofa.