Azam FC Yawasili Zanzibar Kwaajili ya Mapinduzi Cup

Klabu ya Azam FC imetua hii leo jijini Dar es salaam kwaajili ya michuano ya Mapinduzi Cup ambapo wanatarajiwa kukipiga hapo kesho dhidi ya Malindi FC.

 

Azam FC Yawasili Zanzibar Kwaajili ya Mapinduzi Cup

Mchezo huo na Azam FC utapigwa majira ya saa 10:15 jioni huku Kaimu Afisa habari wa timu hiyo Hasheem Ibwe akisema kuwa wameondoka na kikosi kamili na malengo yao yakiwa na kubeba kombe hilo.

Vijana hao wa Kally Ongala wametoka kuchukua pointi tatu kwenye mchezo waowa ligi uliopita kwa kuibugiza Mbeya City FC mabao 6-1 huku mchezaji wao Abdul Sopu akiingia kambani mara mbili.

Azam FC Yawasili Zanzibar Kwaajili ya Mapinduzi Cup

Timu hiyo ya Chamazi ipo nafasi ya tatu huku nafasi ya kutetea taji la NBC likiwa ni vigumu kwahiyo nguvu zao wameziwekeza kwenye michuano iliyobakia ya Mapinduzi na Kombe la Shirikisho la Azam.

 

 

 

Acha ujumbe