Baada ya kuingia katika hatua ya nusu fainali, Kaimu Ofisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe amesema hawaihofii timu yeyote watakayokutana nayo.

Azam tayari wamekata tiketi ya kucheza hatua ya nusu fainali ambapo wanasubiri mshindi wa kundi B kati ya Yanga na Singida Big Stars.

Azam hawaihofii timu yeyote

Ibwe amesema kuwa “Ni kweli mwanzoni hatujaanza vizuri haya mashindano lakini katika mchezo wa pili tulidhamiria kutafuta nafasi ya kuvuka katika hatua ya nusu fainali na tunashukuru tumefanikiwa.

Azam hawaihofii timu yeyote

“Sisi dhamira yetu kubwa ni kuhakikisha tunaingia hatua ya fainali na hatimae kutwaa ubingwa wa michuano ya Mapinduzi kwa mara ya tano na wachezaji wanalifahamu hilo hivyo wapo tayari kupambana.

“Tunamsubiri mshindi kati ya Singida Big Stars na Yanga na yeyote ambaye atakuja mbele yetu basi atakuwa mali yetu na hatumhofii kwani tunahitaji kutimiza malengo yetu ya kurejea na kombe.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa