UONGOZI wa Azam FC umefunguka kumsajili kipa kutoka Ulaya ambaye anakuja kurithi nafasi ya Mathias Kigonya aliyeachwa hivi karibuni.
Akizungumzia usajili wao, Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’ amesema kuwa kipa huyo amesajiliwa kwa ajili ya kuchukua nafasi ya kipa aliyeachwa na atatambulishwa hivi karibuni.
Azam, Azam Wamfuata Kipa Ulaya, Meridianbet
“Usajili wetu umelenga kwenye yale maeneo ambayo yalikuwa na mapungufu kwa msimu uliopita ukiangalia tumeachana na wachezaji kadhaa hivyo wale wanaokuja wanakuja kuchukua nafasi za wale walioondoka.
“Kipa anayekuja ni mkubwa sana na atakapotua hapa itakuwa jambo kubwa sana kwani ni mchezaji anayetoka kwenye ligi kubwa ulaya na anakuja kucheza Azam FC.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa