UONGOZI wa Azam FC umetangaza rasmi kuachana na aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Abdihamid Moallin na msaidizi wake Omary Nasser kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Moallin alitangazwa kuwa kocha mkuu wa Azam FC mwezi Januari 25, 2022 akichukua nafasi ya kocha George Lwandamina ambaye nae aliamua kuvunja mkataba yeye mwenyewe.

Azam FC Waachana na Kocha Wao Moallin

Taarifa kutoka klabuni hapo ambayo ilitumwa kwenye ukurasa rasmi wa klabu hiyo iliandika kuwa:

“Tumefikia makubaliano ya pande mbili na kocha wetu, Abdihamid Moallin, na msaidizi wake, Omary Nasser, kuachia ngazi kama kocha mkuu na msaidizi mtawalia.”

Pamoja na hilo lakini, Uongozi wa Azam FC umeamua kuwaacha walimu hao kuwa sehemu ya klabu hiyo kwenye idara ya ufundi.

“Hata hivyo, makocha hao wataendelea kubaki kama sehemu ya idara ya ufundi klabuni kwetu katika nafasi nyingine ambazo tutazitangaza hapo baadaye”.

Kwa mujibu wa maamuzi hayo ya klabu kunamfanya kocha huyo kuhudumu kwa miezi takribani 8 akiwa kama kocha Mkuu.

Azam FC Waachana na Kocha Wao Moallin

Ikumbukwe kuwa Azam FC tarehe 6 Septemba mwaka huu watakutana na Yanga SC kwenye mchezo wa Ligi kuu mzunguko wa 3, hivyo huenda Azam FC ikacheza mechi hiyo bila kuwa na kocha mkuu.

Azam FC Waachana na Kocha Wao Moallin
Aliyekuwa Kocha wa klabu ya Azam FC- Abdihamid

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa