Azam wapo tayari kupambana na Geita Gold

Baada ya kumaliza mchezo dhidi ya Kagera Sugar, kikosi cha Azam FC kimeelekea mkoani Geita na kuanza mazoezi kwa ajili ya mchezo wao unaofuata na Geita Gold.

Mchezo huo wa ligi kuu unatarajiwa kupigwa Desemba 21 mwaka huu kwenye Uwanja wa Nyankumbu mkoani Geita.

Azam wapo tayari kupambana na Geita Gold

Akizungumza baada ya mazoezi yao yaliyofanyika jana jumatatu, Kaimu Kocha Mkuu, Kalimangonga Ongala alisema kuwa kila kitu kipo sawa kuelekea kwenye huo mchezo.

Azam wapo tayari kupambana na Geita Gold

“Tumefanya mazoezi yetu ya kwanza na mipango yetu kama benchi la ufundi ni kuhakikisha vile tulivyomaliza mechi iliyopita basi kasi ile tuanze nayo.

“Hatuna majeruhi watu wote waliosafiri wapo fiti na wachezaji ambao tuliwaacha Dar ni Ibrahim Ajibu na Shaban Chilunda.”

Acha ujumbe