Uongozi wa klabu ya Azam FC umetangaza rasmi kuachana na kiungo wa kikosi hicho na timu ya Taifa Stars (Tanzania), Mudathir Yahya baada ya mkataba wake kumalizika.

Kikosi cha Azam kwa sasa kipo nchini Misri kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao ambacho kitashiri michuano ya ligi kuu pamoja na ile ya Shirikisho barani Afrika.

Azam, Azam Yaachana Mudathir Yahya, Meridianbet

 

Mudathir ni miongoni mwa nyota ambao walikuwemo kwenye kikosi cha Stars kilichoitoa Somalia hivi karibuni kwenye michuano ya CHAN.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye ukurasa rasmi wa Azam FC zimeeleza kuwa “Tunathibitisha kuachana na mchezaji wetu wa muda mrefu Mudathir Yahya baada ya mkataba wake kumalizika tangu Juni 30 mwaka huu.

“Tunamtakia kila la kheri kwenye kazi yake ya mpira na tunamkaribisha klabuni kwetu wakati wowote.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa