AZAM YAIPIGIA MAHESABU MAKALI NBC

HATIMAYE mabosi wa klabu ya Azam FC, wamelazimika kuanza kuanzisha mikakati mipya ya kuhakikisha wanabeba kombe la Ligi Kuu Bara msimu ujao, kwa kuwataka benchi la ufundi kuhakikisha wanatumia sahihi muda huu wa mapumziko kujinoa na kikamilifu ili ligi inaporudi basi waweze kupata matokeo yatakayowapa ubingwa.

Hadi sasa Azam FC wana pointi sita baada ya kuvuna ushindi kwenye michezo yao miwili dhidi ya Kitayonce na Tanzania Prisons.AZAMMkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Azam FC, Zakaria Thabit ‘Zaka za Kazi’ alisema: “Tayari kikosi kimerejea mazoezini baada tu ya uongozi kukaa na kuweka mikakati mipya ya kuhakikisha tunaenda kubeba kombe la ligi.

“Tutakuwa na michezo kadhaa ya kirafiki na mmoja wapo ni dhidi ya Art Solar ambao tutacheza nao ndani ya wiki ijayo kisha benchi litaangalia mchezo mwingine kutokana na ratiba ili tuweze kuwa sawa kabla ya chochote kile.”

Acha ujumbe