Klabu ya Kagera Sugar imeaikalia kooni klabu ya Azam Fc baada ya kuilazimisha ssuluhu katika mchezo wa kwanza wa mzunguko wa pili ligi kuu ya NBC.

Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Kaitaba klabu ya Kagera Sugar ilionekana kuonesha ubora wa hali ya juu na kufanikiwa kuitangulia klabu ya Azam kupata bao kupitia kwa Yusuph Mhilu mapema tu dakika ya 12 ya mchezo.

Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Kagera Sugar wakiwa nyumbani walikua mbele kwa bao moja kwa bila, Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Wanalambalamba wakitafuta bao la kusawazisha lakini Kagera Sugar waliopata bao la pili kupitia kwa Meshack Abraham dakika ya 62 ya mchezo.azamBaada ya Kagera kua mbele kwa mabao mawili kwa bila klabu ya Azam walitulia na kurudi mchezoni na kuanza kutengeneza mashambulizi ya hapa na pale mpaka pale dakika ya 68 Iddi Suleiman alipoipatia klabu hiyo bao la kwanza la kusawazisha.

Azam waliendeleza msako wa nyani mpaka pale dakika ya 87 kupitia kwa Idris Mbombo alipoisawazishia klabu hiyo na matokeo kuisha kwa mabao mawili kwa mawili, Hivo klabu ya Azam wamedondosha alama mbili katika mchezo wao wa kwanza katika mzunguko wa pili na kuwafanya kufikisha alama 36 wakiwa nafasi ya pili.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa