Kuanzia sasa Azam FC, ikiwa kwenye Uwanja wao wa nyumbani katika michezo ya ligi kuu viingilio ni jezi zao za msimu wowote.

Kikosi hicho kilichosheheni nyota wengi wa kimataifa pamoja na wazawa kama vile Ibrahim Ajibu wanautumia uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar.

Azam, Azam Yaondoa Viingilio Uwanja wa Chamanzi, Meridianbet

Kwa sasa kikosi hicho kinaendelea na maandalizi ya kuiwinda Dodoma Jiji kwenye mchezo wa ligi kuu utakaopigwa kesho jumatano kwenye dimba la Azam Complex.

Akizungumzia hilo, kaimu Ofisa Habari wa Azam, Hasheem Ibwe alisema: “Mechi zote za ligi ambazo Azam FC itacheza kwenye Uwanja wa nyumbani kiingilio itakuwa jezi zetu.

“Utaratibu huo umeanza kuanzia kwenye mechi ya kesho dhidi ya Dodoma Jiji ambapo shabiki hatatoa hela kulipia kiingilio bali jezi haijalishi ni ya msimu gani.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa