Klabu ya Azam Fc imethibitisha kumsajili golikipa wa kimataifa wa Ghana aliyekua anachezea klabu ya Bechem United ya nchini Ghana anayejulikana kama Abdulai Iddrusi.

Klabu ya Azam ambaye dirisha kubwa la usajili ilifanikiwa kumsajili golikipa wa kimataifa Comoro ambaye aliwahi kukipiga katika ligi kuu nchini Ufaransa Ally Ahmada, Lakini matajiri a jiji la Dar-es-salam wameamua kuongeza golikipa mwingine wa kimataifa.azamKiwango kilichooneshwa na golikipa wasasa klabuni hapo Ally Ahmada ni miongoni mwa sababu za uongozi wa klabu ya Azam kuamua kuingia sokoni na kutafuta golikipa mwingine, Kiwango cha  Ahamda kimekua hakiridhishi kwa siku za hivi karibuni.

Matajiri wa jiji la Dar-es-salam walimuacha golikipa wao namba mbili klabuni hapo Ahmed Salula wiki kadhaa nyuma, Hivo walihitaji pia mbadala wa golikipa Ally Ahmada kama ikitokea akaumia awepo golikipa mwenye ubora mkubwa.azamKlabu ya Azam ambayo imefanikiw kuingiza timu kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la mapinduzi visiwani Zanzibar, Imesajili golikipa kuotoka nchini Ghana kwajili ya kuboresha safu ya ulinzi ya klabu hiyo ambayo inaonekana kusuasua siku za hivi karibuni.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa