Aziz Ki Ampagawisha Kocha Azam

BILA kupepesa macho, Kocha Mkuu wa Azam FC Bruno Ferry, alisema wazi kuwa nyota wa Yanga Aziz Ki Stephen ni mchezaji hatari sana na ndiye aliyeivuruga safu yake ya ulinzi juzi pale kwa Mkapa.

Ferry alisema, Aziz Ki alifanya mambo makubwa sana kwenye mchezo ule, alikuwa anafanya anachotaka na aliwafanya walinzi wake wakose uhuru na utulivu.aziz ki“Amefanya makubwa sana, amecheza mchezo mkubwa, aliwavuruga sana walinzi wangu, ni mchezaji mwenye daraja la juu na alifanikiwa kwenye kila alichofanya uwanjani,” alisema.

Ferry akaongoza kuwa kilichowaangusha ni kushindwa kudhibiti mchezo baada ya kuongoza 2-1 mbele ya Yanga na kufungwa 3-2 baada ya dakika 90, ni kutokana na kukosa uzoefu kwa wachezaji wake.aziz ki“Tulicheza na timu kubwa, timu yenye wachezaji bora, walikosa utulivu na kusahau kuwa wanacheza na timu kubwa.”

Acha ujumbe