Kiungo wa klabu ya Yanga mwenye thamani zaidi Stephane Aziz Ki ametaja wachezaji wanaomvutia na kumfanya kupenda kucheza soka.

Kiungo huyo mwenye ubora mkubwa amesema kuna wachezaji waliomvutia zaidi kupenda mpira wa miguu na pengine kutaka kuucheza kabisa na anatamani kufika ambapo wamefika wao.aziz kiAziz Ki anavutiwa zaidi na Lionel Messi, Luca Modric, pamoja na Juan Roman Riquelme na nyota hao ndio wamemvutia mchezaji huyo kupenda mpira wa miguu na kutamani kuucheza kabisa. Kiungo huyo anatamani siku moja kufikia ubora wa wachezaji hao ambao wamemvutia kuupenda mchezo huo.

Pia kiungo amefunguka sababu ya yeye kuwapenda wachezaji hao ni kutokana na nafasi wanazocheza ndizo zimefanya kuwapenda kwakua wachezaji hao wanacheza namba 10 uwanjani na ndio nafasi Aziz Ki anapenda kuicheza zaidi uwanjani.aziz kiMchezaji huyo bora wa msimu uliopita wa ligi kuu nchini Ivory Coast amecheza kwenye kiwango kizuri ndani ya klabu ya Yanga.Ikiwa Japo bado hajaonesha ubora aliokua nao ndani ya klabu yake ya zamani ya Asec Mimosas.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa