AZIZ KI KWENYE UBORA WAKE

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga Aziz KI kasi yake ya kucheka na nyavu imezidi kuwa bora akizipa tabbu nyavu kwenye mechi ambazo anacheza ndani ya uwanja msimu wa 2023/24.

Tayari amefunga mabao 13 akiwa namba moja kwa wakali wenye mabao mengi ndani ya ligi anafuatiwa na Feisal Salum wa Azam FC huyu katupia mabao 12 kibindoni.AZIZ KIAziz KI ni chaguo la kwanza kwa Miguel Gamondi amekuwa na mwendelezo bora katika kufunga na kutoa pasi za mabao akiwa kafikisha jumla ya mabao 13 na pasi alizotoa ni sita.

Ipo wazi kwamba kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Ihefu uliochezwa Uwanja wa Azam Complex wakati ubao ukisoma Yanga 5-0 Ihefu alitoa hat trick ya pasi na kufunga bao moja hivyo alihusika kwenye mabao manne kati ya matano.

Bao lake la 13 alifunga kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Geita Gold uliochezwa Uwanja wa Azam Complex ilikuwa Machi 14 dakika ya 28 akitumia krosi ya Okra Magic ambaye anatoa pasi yake ya kwanza kwenye ligi msimu wa 2023/24 akiwa na uzi wa Yanga.AZIZ KIAziz KI kahusika kwenye mabao 19 kati ya 48 yaliyofungwa na Yanga akiwa kafunga 13 na kutengeneza pasi za mabao 6 msimu wa 2023/24 kwenye ligi.

Acha ujumbe