KILA mmoja anamtaja staa wa Yanga raia wa Burkinafaso Stephen Aziz Ki kuwa ndiye bora zaidi kwenye kikosi hicho baada ya kufunga mabao matatu jana dhidi ya Azam FC.

Kila mchambuzi na aliyeutizama mchezo wa Yanga na Azam FC uliochezwa kwenye Uwanja wa Mkapa na Yanga kushinda 3-2, anatajwa sana Aziz Ki juu ya ubora wake. Lakini mwenyewe Azizi Ki ana majibu tofauti. Akizungumza baada ya mchezo huo uliochezwa jana Jumatatu Stephen alisema, siyo ubora wake pekee ndiyo sababu ya Yanga kushinda mchezo ule, bali ni ubora wa timu ya Yanga na wachezaji wote wa timu hiyo.

“Siyo mimi, bali ni ubora wa timu yetu, Yanga kwa sasa inacheza vizuri zaidi, inacheza kwa maelewano na kila mtu ni bora sana hapa, hayo yote yanafanya kwa pamoja tunapata matokea mazuri,”alisema.

Kwa sasa Aziz Ki ndiye kinara wa mabao akiwa amefunga mara sita na kutoa assit mbili. Chini yake yupo Jean Baleke wa Simba mwenye mabao matano, Feisal ana mabao manne.JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa