Kiungo mshamuiaji wa Yanga Azizi KI amesema kuwa anapenda kufunga ama kutengeneza nafasi za mabao akiwa ndani ya uwanja.

Nyota huyo ni ingizo jipya ndani ya Yanga ambapo alijiunga na kikosi hicho akitokea ASEC Mimosas.

Oktoba 23,2022 alifunga bao la pili ndani ya ligi ambapo alimtungua Aishi Manula kwa pigo la faulo akiwa nje ya 18.

Mchezo huo ulikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1 na kuwafanya wagawane pointi mojamoja.

Nyota huyo amesema:”Ninapenda kufunga na kutengeneza nafasi za mabao nina amini kwamba mashabiki wanapenda kuona haya yanatokea.

“Kikubwa ni ushirikiano na kila mmoja anafanya kazi yake kutimiza majukumu yake hivyo mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi”

Leo Yanga ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa ligi dhidi ya KMC ambao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa saa 1:00 usiku.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa