KLABU YA Simba SC Imemtambulisha rasmi Kiungo wa Ulinzi Yusuph Kagoma mwenye umri wa miaka 28 kwa mkataba wa miaka mitatu, utakaodumu hadi msimu wa 2026/2027. Jisajili hapa kuwa wa kwanza kushinda Mamilioni ya Meridianbet kila siku.
Yusuph Kagoma alikuwa anahusishwa zaidi na watani zaoYanga, kabla ya upepo kubadilika na kijana huyo kusaini mkataba na Simba, hali ya kuwa tayari alikuwa kishasinya mkataba wa awali na Yanga.
Beti na Meridianbet kwa ushindi mkubwa na odds kubwa, Ligi zinakaribia kuanza, usije kupishana na gari la Mshahara.
Inasemekana kwamba Dau kubwa la pesa lililowekwa na Simba, ndio lilimvutia zaidi Kagoma, hadi kuoma kusaini mkataba rasmi na Yanga na kuwaomba Viongozi wake wa Singida Fountain Gate kurudisha pesa za Yanga.
Sehemu ya Taarifa ya Simba kutoka Simba App iliandika kwamba, Yusuph Kagoma ni seemu ya mpango wa Simba kurudisha ubora wao.
“Kiungo mkabaji, Yusuph Kagoma ni mchezaji wetu mpya baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu ya kukitumikia kikosi chetu kutoka Singida Fountain Gate.”
“Kagoma ni moja ya vijana wazawa wenye uwezo mkubwa wa kuzuia timu ikishambuliwa na kupandisha mashambulizi.”
“Uwezo wake na umri wake ni miongoni mwa vigezo vilivyotuvutia kutafuta saini yake na tuna matarajio makubwa kutoka kwake.”
“Kagoma yupo kwenye mipango ya maboresho makubwa ya kuirejesha timu katika ubora ambao mashabiki wetu wanatamani kuiona.”
Baada ya kukamilika kwa usajili huu wa Yusuph Kagoma, sasa safu ya Viungo ya Simba inakuwa na wachezaji 6, ikiongozwa na Mzawa Mzamiru Yassin, Fabrice Ngoma, usajili mpya ni Augustine Okejepha kutoka Rivers Utd, Deborah Fernandes, Jean Charles Ahoua na YUsuph Kagoma.
Simba inatarajiwa kuanza safari ya kuelekea Misri kwaajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2024/25.
Michezo ya Kasino na Sloti ni machimbo yanayotoa pesa kirahisi. Cheza kasino hapa.