Baada ya Al Ahly Kutua, Simba Watoa Tamko

BENCHI la ufundi la Simba limebainisha kuwa litawaongezea dozi wachezaji wao kwenye uwanja wa mazoezi kuwa imara zaidi katika mechi wanazocheza ikiwa ni pamoja na safu ya ulinzi ambapo moja ya michezo inayowakabiri ni dhidi ya Al ahly mchezo wa kwanza hatua ya robo fainali. Jisajili na Meridianbet upate bonasi za kasino kibao na odds kubwa za ubashiri kwa machaguo kibao.

 

AL AHLY

Hiyo inakuja Baada ya Wapinzani wao Al Ahly kutua mapema hii leo wakiwa wamejikoki Ili kuondoka na ushindi kwenye mchezo huo.

Ipo wazi kwamba ndani ya Ligi Kuu Bara, safu ya ulinzi ya Simba imekuwa na mwendo mbovu katika ulinzi ndani ya timu tatu zilizo kwenye tatu bora msimu wa 2023/24.

Seleman Matola, kocha msaidizi wa Simba amesema kuwa wanatambua makosa yalipo jambo linalowafanya wafanye kazi kwa umakini kuelekea kwenye mechi zijazo kwa kuwaongezea wachezaji wao dozi nyingine. Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.

“Unaona kwenye mechi ambazo tunacheza tunapata ushindi na wakati mwingine tunawapa ruhusa wapinzani kutufunga huwa tunaongea na wachezaji na tutaongeza dozi nyingine kwenye uwanja wa mazoezi.

“Kikubwa ni kuwa makini kwa kuwa mchezo wa mpira ni mchezo wa makosa, kuelekea kwenye mechi zetu zijazo tuna imani tutakuwa imara hilo linawezekana kutokana na wachezaji kujituma na kutimiza majukumu yao kwa ushirikiano,”.

Kikosi cha Simba baada ya kucheza mechi 19 ndani ya ligi ni mabao 18 ukuta umeruhusu ikiwa namba moja kwa timu ambazo zimefungwa mabao mengi ndani ya tatu bora msimu wa 2023/24.

Mchezo ujao kwa Simba ni wa Ligi ya Mabingwa Afrika itakuwa dhidi ya Al Ahly unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Machi 29. Odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni njia rahisi ya kukupa mtonyo mrefu. Ingia mchezoni hapa.

Acha ujumbe