BALEKE KWENYE MIPANGO YA KUONGEZA MKATABA SIMBA

Klabu ya Simba inaelezwa ipo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha dili la kumsajili mshambuliaji wa klabu hiyo Jean Othos Baleke kwa kumpa mkataba wa kudumu klabuni hapo.

 

BALEKE KWENYE MIPANGO YA KUONGEZA MKATABA SIMBA

Inafahamika kua mshambuliaji Jean Baleke yupo kwa mkopo klabuni hapo akitokea Tp Mazembe ya nchini Congo, Lakini Simba wanaelezwa wako mwishoni kumalizana na mshambuliaji huyo na kumpa mkataba wa kudumu.

Mazungumzo baina ya Wekundu wa Msimbazi na Tp Mazembe yameenda vizuri na ndio sababu ya klabu hiyo kufikia katika hatua nzuri na mshambuliaji huyo raia wa kimataifa wa Congo.

BALEKE KWENYE MIPANGO YA KUONGEZA MKATABA SIMBA

Jean Baleke amekua na kiwango bora sana ndani ya klabu ya Simba tangu ajiunge na klabu hiyo katika dirisha dogo la mwezi Januari msimu uliomalizika, Jambo lililowavutia kutaka kumpa mkataba wa kudumu aendelee kusalia kwenye viunga vya Msimbazi.

Klabu ya Simba inahitaji kufanya maboresho klabuni hapo katika dirisha dogo la mwezi Januari, Hivo klabu inahitaji kuwapa mikataba wachezaji wake ambao wanamaliza muda wao klabuni lakini pia kuongeza wa nje ya klabu hiyo.

Acha ujumbe