KLABU ya Yanga SC imeweka rekodi tamu kwa upande safu yake ya ulinzi baada ya kufanikiwa kucheza mechi zote mbili za kimataifa, ambazo ni sawa na dakika 180 bila kuruhusu bao katika hatua za awali mbele ya Zalan FC.

 

Beki za Yanga SC Zaweka Rekodi Kimataifa

Mchezo wa kwanza nyota wa Young Africans ikiwa ni pamoja na Dickosn Job, Bakari Mwamnyeto, Kibwana Shomari hawakuokota bao sawa na ule wa pili, yote ilichezwa Uwanja wa Mkapa.

Ni mabao 9 wameweza kufunga Young Africans na kinara wao ni Fiston Mayele ambaye katupia mabao 6, kwenye kila mchezo alitupia hat trick.

 

Beki za Yanga SC Zaweka Rekodi Kimataifa

Ushindi huo unaifanya Young Africans, kusonga mbele hatua inayofuata na wanatarajiwa kukutana na Al Hilal ya Sudan hatua inayofuata.

Wakipenya hapo safari inaelekea katika hatua ya makundi ndani ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Nasreddine Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa ushirikiano na kufuata maelekezo ni mambo yanayowapa matokeo.

 

Beki za Yanga SC Zaweka Rekodi Kimataifa

“Kila mchezaji anajua kazi yake na wanashirikiana, kikubwa ni kuona tunapata matokeo kwenye mechi ambazo tunacheza,”.

Mchezo wa pili jana Septemba 17, timu hiyo ilishinda mabao 5-0 ambapo Mayele alifunga matatu, Farid Mussa na Aziz KI hawa walitupia mojamoja.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa