Benchika Afunguka Kilichoiondoa Simba Ligi ya Mabingwa

KOCHA Mkuu wa Simba Abdelhack Benchika amesema kuwa sababu kubwa yakutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ni ubora wa Wapinzani wao hao. Jisajili na Meridianbet upate bonasi za kasino kibao na odds kubwa za ubashiri kwa machaguo kibao.

 

Simba

Kocha mkuu wa klabu ya simba abdelhack Benchika aweka wazi sababu ya timu yake kutolewa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa afrika kwenye hatua ya robo fainli dhidi ya Al Ahly kuwa walikuwa bora na uzoefu ndivyo vilivyopelekea klabu hiyo yenye maskani yake mtaa msimbazi kupoteza, huku akikubali kuwa walikosea mchezo wao wa nyumbani.

Simba pamoja na mashabiki wake walikuwa na matumaini makubwa ya kuwatoa Al Ahly na kufuzu hatua ya nusu fainiali ya mashindano ya klabu bingwa barani Afrika kwa mara ya kwanza tokea kuanzishwa kwa mashindo haya rasmi tokea kuanzishwa kwake rasmi na kupewa jina la klabu bingwa barani afrika, Awali simba ilishawai fika hatua ya fainali kwenye michuano la vilabu afrika lililojulikana kama Abiola cup huku Simba ikipoteza kwa goli mbili bila dhidi ya stella abidjan yenye makazi yake nchini Ivory Coast.

BENCHIKHA alisema: “Tumecheza na timu yenye uzoefu hata sehemu kubwa ya wachezaji wao wana uzoefu wa CAFCL, ila pia nimeridhika na mtusamehe sana mashabiki wetu wa Simba, maana tuliikosea mechi hapa nyumbani Tanzania.

“Kule tulicheza vizuri hasa kipindi cha kwanza tulicheza vizuri sana japo tulikosa nafasi mbili za magoli kipindi cha kwanza, na kipindi cha pili tuliruhusu bao dakika ya pili tu, ligi ya CAFCL sio kama mechi za ligi inahitaji uzoefu pia hasa hatua kama hizi uzoefu pia unachangia kwa wachezaji.”

Klabu ya simba kwa sasa inarejesha nguvu zake kwenye ligi kuu ya Tanzania bara NBC Premier ligi huku wakijianda na mchezo wao wa FA dhidi ya Mashujaa tarehe tisa kwenye uwanja wa lake Tanganyika kigoma. Odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni njia rahisi ya kukupa mtonyo mrefu. Ingia mchezoni hapa.

 

 

Acha ujumbe