KOCHA wa Simba Abdelhack Benchikha amesema kuwa bado anapata ugumu kwenye mechi zake kwa kuwa timu nyingi hazifahamu na analazimika kuzisoma kwanza kipindi cha kwanza.
Benchika amesema hayo kufuatia ushindi wa mabao 2-0 waliopata Jana dhidi ya Singida Fountain Gate FC kwenye Kombe la Mapinduzi.“Leo (Jana) nimefanikiwa, tofauti na mwanzo nilivyosema sikufanikiwa ila leo nimefanikiwa, unajua mimi ni mgeni hapa kwa hivyo nakosa baadhi ya taarifa za namna ya timu zinavyocheza.“Ndio maana huwa nawasoma kipindi cha kwanza na kipindi cha pili huwa nawajua na kufanya masahihisho, kama ningekuwepo hapa miezi mitatu au sita ningekuwa najua namna ya baadhi ya timu zinavyocheza hapa Tanzania na isingekuwa inanisumbua.”Alisema Benchikha