BENCHIKHA ANATAKA REKODI YA KUKUMBUKWA SIMBA

KOCHA wa Simba, raia wa Algeria Abdelhack Benchikha amesema kuwa kwenye moyo na akili yake Kuna kitu kimoja kinachoitwa Simba kwenda nusu fainali ikiwa kwenye mikono yake.

Benchikha amefunguka kuwa, Kila mtu ana namna yake kuelekea kwenye mchezo huo wa kesho dhidi ya Al Ahly, lakini yeye anataka kuvunja mfupa uliomshinda fisi.BENCHIKHA“Najua kuwa Kila mmoja ana namna yake anayofikiria kuelekea kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Al Ahly. Mimi nataka rekodi na historia ya kuwa Kocha wa kwanza kwenda nusu fainali na Simba.

“Nataka kuivusha Simba kwenye hatua hii ya robo fainali na kwenda nusu fainali, hayo ni malengo yangu na yetu sisi hadi wachezaji, nataka twende mbele zaidi tofauti na ambapo Simba huwa inafikia.BENCHIKHA“Safari hii nataka kuivusha Simba na najua wachezaji wangu wapo tayari,” amesema Benchikha.

Acha ujumbe