JE una cheti cha kidato cha nne na unaweza kufundisha mpira? basi Biashara United panakufaa kwa sababu wanahitaji kupata Kocha Mkuu kwenye kikosi chao.

Taarifa rasmi iliyotolewa na Biashara United ambayo ilishuka ligi Kuu bara msimu wa 2021/22 na msimu ujao wa 2022/23 itashiriki Championship imebainisha vigezo vinavyotakiwa.

Biashara United

Sifa hizo kwa mwombaji ni pamoja na kuwa raia wa Tanzania, awe na elimu ya kidato cha nne na cheti, awe na elimu ya ukocha wa leseni A au B ya Caf. Awe mtu anayetambua majukumu yake kwa wachezaji viongozi na mashabiki wa timu.

Pia sifa nyingine ni umri usiopungua miaka 25 na kuendelea na awe na akili timamamu na awe mwaminifu na kufanya kazi kwa bidi kutimiza malengo ya Biashara United.

Hivi karibuni klabu ya Biashara ili pata pigo la viongozi wake walijiuzuru, baada ya klabu hiyo kushukuka daraja msimu ulioisha kwenye kikao cha dharula kilichofanyika July 11.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa