UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa hesabu zao kubwa kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika ni kutinga hatua ya nusu fainali.
Simba chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliveira imetinga hatua ya makundi kwa kuwafungashia virago Power Dynamos ya Zambia kwa kanuni ya faida ya bao la ugenini kwani mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Zambia ubao ulisoma Power Dynamos 2-2 Simba na ule wa pili jijini Dar es Salaam Simba 1-1 Power Dynamos.Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally alisema kuwa kazi kubwa katika anga la kimataifa ni kupambana kufikia hatua ya robo fainali.
“Kila timu ina malengo na tunatambua kwamba wapinzani wetu ambao wapo imara tutapambana nao ili kupata matokeo yatakayotupa nafasi kufikia malengo ya kutinga hatua ya robo fainali.“Ni mechi ngumu za kimataifa hilo lipo wazi, lakini tunaamini wachezaji waliopo pamoja na benchi la ufundi kazi yao itakuwa kubwa. Kila mmoja shauku yake ni kuona tunasonga mbele hilo litafanikiwa na mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,” alisema Ahmed Ally.