CHAMA AISHITAKI SIMBA TFF

INAELEZWA kuwa kiungo mpya wa Yanga, Clatous Chama amefungua shauri kwenye mamlaka ya soka nchini akidai kuwa waajiri wake wa zamani hawajampa release letter ambayo itampa uhalali wa kuichezea Klabu ya Yanga.

Klabu ya Simba inaelezwa kuwa imekataa kumpa release letter Chama ikidai aliondoka kinyume cha utaratibu kwenda Yanga.

Shauri la Chama litasikilizwa leo 16 Julai 2024 pamoja na lile la Lameck Lawi mchezaji wa Coastal Union msimu wa 2023/24.CHAMALawi alitambulishwa ndani ya kikosi cha Simba kuwa ingizo jipya akitokea kikosi cha Coastal Union ambapo alikuwa hapo kwa msimu wa 2023/24.

Ndani ya ligi Lawi alicheza jumla ya mechi 25 akikomba dakika 2,230 alikuwa chaguo la kwanza kwenye benchi la ufundi la Coastal Union.

Baada ya kutambulishwa Simba, uongozi wa Coastal Union ulibainisha kuwa bado mchezaji huyo ni mali ya Coastal Union wanahitaji kuwa naye kwenye mashindano ya kimataifa ambapo Coastal Union inashiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

Acha ujumbe