KIUNGO mshambuliaji wa Simba SC ambaye ni raia wa Zambia Clatous Chama amesema kuwa jana haikuwa siku nzuri kazini hivyo watarejea vizuri kama kawaida.

Simba SC walipoteza mchezo wa jana dhidi ya Azam FC kwa bao 1-0 goli lililofungwa na Prince Dube dakika ya 35, baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa kiungo Akaminko na kumchungulia mlinda mlango Aish Manula na kuutia kimiani.

 

Chama Anena Jambo Baada ya Kipigo na Azam FC

Chama aliandika ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa Twitter masaa machache baada ya mchezo huo, akisema kuwa “haikuwa siku nzuri kazini hivyo watarejea vizuri kama kawaida”


Matokeo hayo ya jana yanaifanya Simba SC kuwa nafasi ya 3 kwa alama 14 nyuma ya Mtibwa Sugar wenye alama 15 na michezo 9 huku Yanga SC akiwa kileleni mwa Ligi kwa alama 17 huku wakiwa na michezo 7 sawa na mtani wake Simba SC.

Chama amekuwa na kiwango bora zaidi tangu aliposajiliwa na Simba SC mwaka 2017 na amekuwa akiwaka sana mitaa ya Msimbazi, hali iliyomfanya ASAJILIWE na klabu ya nchini Morocco, RS Berkane lakini hakufanikiwa kuonesha makali yake na kurejea tena Simba katikati ya msimu ulioisha.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa