Chama Ashinda Goli Bora la Wiki CAF

Kiungo wa klabu ya Simba Clatous Chota Chama amefanikiwa kushinda kinyang’anyiro cha goli bora la wiki katika michuano ya ligi ya mabingwa Afrika katika mzunguko wa tano wa michuano hiyo.

Chama ameshinda kinyang’anyiro hicho akishindana na wachezaji mbalimbali kama Mahmoud Kahraba, na Percy Tau wote wa Al-Ahly ya nchini Misri, Lakini kiungo huyo wa Simba amefanikiwa kushinda baada ya goli lake la mpira wa adhabu alilofunga dhidi ya Horoya kuongoza kwa kupigiwa kura.ChamaKiungo huyo alikua na kiwango bora sana katika mchezo na kufanikiwa kufunga mabao matatu huku goli moja likifanikiwa kushinda bao bora la la wiki katika michuano hiyo, Lakini vilevile staa huyo wa kimataifa wa Zambia ameingia kwenye kikosi bora cha wiki kwenye michuano hiyo.

Chama mbali na kushinda bao bora la wiki katika michuano hiyo lakini vilevile amechaguliwa kuwania uchezaji bora wa wiki kwenye michuano hiyo akishindana na Mahmoud Kahraba, Percy Tau ambao wanakipiga katika klabu ya Al-Ahly ya Misri.ChamaKiungo Chama amekua kwenye kiwango bora sana kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Afrika, kwani mpaka sasa anaongoza kwenye ufungaji wa ligi hiyo akiwa na mabao manne mpaka sasa na mpaka sasa mchezaji huyo ameshafanikiwa kushinda kinyang’anyiro cha mchezaji bora wa wiki wa michuano hiyo kwenye mzunguko wa nne.

Acha ujumbe