Kiungo fundi wa klabu ya soka ya Simba raia wa kimataifa wa Zambia Clatous Chota Chama amefanikiwa kujiunga na wenzake kwenye kambi fupi ya klabu hiyo iliyopo nchini Dubai mapema leo.

Kiungo Chama alipata likizo fupi kwenye kipindi cha sikukuu na kuelekea nchini kwao Zambia, Jambo lililomfanya kiungo huyo fundi kushindwa kwenda na wenzake nchini humo na ikumbukwqe pia kiungo huyo hakuwepo kwenye kikosi kilichoshiriki kombe la mapinduzi.chamaKlabu ya Simba iliondoka nchini Tanzania siku ya tarehe 7 mwezi huu na kuelekea nchini Dubai ambapo wameweka kambi fupi ya siku saba kama mabavyo taarifa ya klabu hiyo ilivyoeleza. Hivo kiungo huyo amefanikiwa kujiunga na klabu hiyo siku ya nne ya mazoezi wakiw nchiniĀ  humo.

Clatous Chama ndio mchezaji pekee aliekua mzima ambaye hakusafiri na timu hiyo siku ya kwanza timu hiyo ilipoelekea Dubai kuweka kambi fupi, Lakini rasmi leo kiungo huyo fundi ameweza kujumuika na wenzake kwenye kambi ya mazoezi ya klabu hiyo Dubai.chamaKlabu ya Simba imeweka kambi fupi ya siku saba nchini Dubai ambayo watakaa kwa siku saba kwajili ya kujiandaa na michuano inayowakabili siku za usoni, Lakini mwekezaji huyo aliweka wazi kua lengo kubwa pia la kuweka kambi Dubai ni wachezaji wa timu hiyo kuweza kumuelewa vizuri kocha mpya wa klabu hiyo Roberto Oliviera.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa