Mchezaji wa timu ya Simba Cloutus Chota Chama na mchezaji wa Yanga Stephan Aziz Ki wamefungiwa michezo mitatu (3) ya ligi kuu Tanzania Bara kutozwa faini ya shilingi laki tano (500,000) kwa kosa la kukwepa kusalimiana na wachezaji wa timu pinzani kabla ya kuanza kwa mchezo wao.

 

Chama na Azizi Ki Wala Rungu TFF

Chama na Aziz hawakusaliana na wachezaji wa timu zao pinzani kwenye Dabi ya Kariakoo ya 23 Oktoba iliyopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa na kumalizika mchezo huo kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Wachezaji hao kwa nyakati na mazingira tofauti walionekana kufanya hila kwa kusubiri nje ili kusubiri zoezi la kusalimiana likamilike ili waingie kiwanjani na baada ya TFF kujiridhisha na hilo ndipo wameamua kutoa adhabu hiyo.

Chama na Azizi Ki Wala Rungu TFF

Aziz na Chama hawatacheza michezo ya hapa ndani tu ya Ligi kuu lakini ya Kimataifa wataendelea kama kawaida ambapo kwa upande wa Yanga wao watakipiga kesho dhidi ya Club Africain na Simba watacheza dhidi ya Singida Big Stars.

Chama atakosa mechi ya Singida, Ihefu na Namungo, wakati kwa upande wa Aziz Ki yeye atakosa mechi ya Kagera Sugar, Singida na Dodoma Jiji.


AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa