Baada ya Simba kupoteza mchezo wake jana dhidi ya Al Dhafra ya Uarabuni, leo hii itacheza mchezo wake wa mwisho wa kirafiki dhidi ya CSKA Moscow ya Urusi na kuona kama atapata nini saa 10:00 jioni.

Simba imefungwa na kibonde wa Ligi kwa bao 1-0, ambaye kwenye mechi zake 12 ameshinda moja na kutoa sare moja huku akipoteza mechi kumi. Leo anacheza na timu ambayo kwenye ligi yao ipo nafasi ya 5.
Kwenye michezo 17 iliyocheza imeshinda michezo 8, imeenda sare mara 5 na kupoteza michezo yake 4, ikijikusanyia pointi 29 huku akiachwa pointi 13 na kinara wa ligi hiyo Zenit mwenye pointi 42.

Timu hiyo imetoka kupoteza michezo yake miwili mfululizo, huku mechi yake inayofuata atamenyana dhidi ya Orenburg ambayo ipo nafasi ya 7 yenye pointi 25.
Simba na kocha wake mpya Mbrazil wanamalizia mchezo huo kabla ya kurejea jijini Dar es salaam kwaajili ya mchezo wao wa Ligi dhidi ya Mbeya City.


