Clara Luvanga (19 Yrs) Ameorodheshwa Katika Orodha Ya Wachezaji 25 Bora Wa Kike Chipukizi Waliozaliwa Kuanzia Mwaka 2005 …
Katika Orodha Hiyo Clara Ameshika Nafasi Ya 16 Kati Ya Wachezaji 25 Bora Chipukizi Duniani.Katika Orodha Hiyo Ni Wachezaji Wawili Tu Toka Afrika Ambao Wamefanikiwa Kuingia katika Orodha Hiyo Ambao Ni Mtanzania Clara Luvanga Aliye Katika Nafasi Ya 16 Ambaye Anacheza Katika Klabu Ya Al Nassir Ya Saudi Arabia Pamoja Na Msenegali Hapsatou Malado Diallo Ambaye Anacheza Katika Klabu Ya Eibar Ya Hispania.
Nyota Inazidi Kuwa Kali Sana Kwa Clara Baada Ya Kuzidi Kuingia Katika Rekodi Mbalimbali Za Soka La Wanawake Duniani Lakini Pia Katika Vichwa Vokubwa Vya Soka La Wanawake Ulimwenguni.Clara Luvanga Anakuwa Mchezaji Wa Kike Wa Kwanza Toka Tanzania Kuipeperusha Bendera Ya Nchi Katika Rekodi Kubwa Za Soka La Wanawake Ulimwenguni.