Kiungo wa Simba Cloutus Chota Chama ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa Ligi wa mwezi Desemba kutokana na kiwango bora ambacho amekionyesha ndani ya mwezi huo.

 

Cloutus Chota Chama Mchezaji Bora Mwezi Desemba

Chama ndani ya mwezi Desemba amecheza mechi tano na amefunga mabao mawili, huku akitoa pasi za mabao matano huku kukiwa hamna mchezaji kutoka timu yoyote amefanya hivyo ndani ya mwezi huo.

Cloutus Chama amemshinda John Bocco na Fiston Mayele wa Yanga ambao walikuwa wakiwania tuzo hiyo huku TFF wakimchagua kiungo huyo kutokana na ubora wake aliouonyesha.

Cloutus Chota Chama Mchezaji Bora Mwezi Desemba

Licha ya tuzo hizo lakini bado Simba ipo nafasi ya pili baada ya kujikusanyia alama zao 44 baada ya michezo yao 19 waliyocheza huku wakiachwa pointi 6 na kinara wa Ligi ambaye ni Yanga.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa