Klabu ya Coastal Union kutoka mkoani Tanga imefanikiwa kupata alama tatu dhidi ya timu ya Singida Big Stars kwenye mchezo wa NBC uliopigwa katika dimba la Liti Mkoani Singida.
Klabu ya Coastal Union maarufu kama wanamangushi wamefanikiwa kupata alama tatu muhimu baada ya kushuhudia wakicheza michezo mitano kwenye ligi kuu ya NBC bila kupata matokeo ya alama tatu.Mchezo huo ambao klabu ya Singida Big Stars ilipewa nafasi kubwa zaidi ya kupata matokeo katika mchezo kutokana na ubora wa kikosi chake pamoja na mfululizo wa matokeo wa klabu ya Coastal Union siku za karibuni, Lakini Wanamangushi wameonesha ubora na kupata matokeo mazuri katika mchezo huo.
Mabao ya Emery Nimuboma pamoja na Vicent Abubakar ndio yaliitenganisha klabu ya Singida Big Stars na alama tatu muhimu huku bao pekee la kufutia machozi la klabu ya Singida likifungwa na Deus Kaseke.Klabu ya Coastal Union wanaongeza alama kutoka alama 12 mpaka kufikia alama 15 msimu huu baada ya kucheza michezo 15 kwenye ligi kuu ya NBC huku wakitoka kupata matokeo mabaya kwenye kwenye mechi tano mfululizo