Klabu ya Coastal Union imesema inausubiri Uongozi wa Simba wakae meza moja kulimaliza pembeni sakata la usajili wa beki Lameck Lawi ambaye shauri lake lilikuwa kkamati ya usuluhishi ya TFF. Jisajili hapa kuwa wa kwanza kushinda Mamilioni ya Meridianbet kila siku.
Ikumbukwe baada ya Simba kupeleka malalamiko yao kwa Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), juu ya sakata hilo la usajili.
Simba na Coastal Union zilitakiwa kukaa meza moja na kumalizana juu ya usajili wa mchezaji huyo ambaye Simba wanadai wamemsajili kihalali huku Coastal Union wakikana kwa kile wanachodai wenzao hao hawakufuata makubaliano yao.
Beti na Meridianbet kwa ushindi mkubwa na odds kubwa, Ligi zinakaribia kuanza, usije kupishana na gari la Mshahara.
Msemaji wa Coastal Union, Abbas El Sabri, alisema jana kuwa wao wanawasubiri mezani Simba kama walivyoshauri kamati hiyo ya TFF.
“Ni kweli tulipewa ushauri huo, sisi hatuna shida tunawasubiri wenzetu wa Simba watakapokuwa tayari tukutane kulimaliza suala hili, kama tulivyosema awali sisi hatua shida, Simba wakiwa tayari tutaenda kukutana nao,” alisema El Sabri.
Hata hivyo, El Sabri alikiri licha ya mchezaji huyo kumworodhesha kwenye usajili wao msimu ujao, kwa sasa yupo nje ya nchi kwa mambo yake binafsi.
“Lawi yupo Ubelgiji kwa mambo yake binafsi, lakini ni mchezaji wa Coastal na tumepeleka jina lake CAF kwa ajili ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ambayo tutashiriki msimu ujao,” alisema El Sabri.
Kwa upande wake, Msemaji wa Simba, Ahmed Ally, alisema kuwa suala hilo linashughulikiwa na uongozi wa juu wa klabu hiyo.
Michezo ya Kasino na Sloti ni machimbo yanayotoa pesa kirahisi. Cheza kasino hapa.
This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.
Strictly Necessary Cookies
Strictly Necessary Cookie should be enabled at all times so that we can save your preferences for cookie settings.
If you disable this cookie, we will not be able to save your preferences. This means that every time you visit this website you will need to enable or disable cookies again.