COASTAL UNION WAMEYATIMBA KWA SIMBA

SAKATA la aliyekua beki wa Coastal Union  Lamek Lawi limeendelea kuchukua sura mpya Baada ya Uongozi wa Simba kupitia Kwa Crescentius Magori ambaye ni mjumbe wa bodi ya Simba SC kupasua ukweli.

Magori ameiambia Meridian Sports kuwa Lawi ni Mchezaji wao halali Baada ya kufuata Utaratibu wote wa uhamisho wa Mchezaji na wanachofanya Coastal ni kukiuka Utaratibu.COASTAL UNION“Ndio tulichelewa kumaliza pesa,. tulilipa nusu lakini mpaka June tulikuwa tumemaliza kulipa pesa yoye ya usajili”

“Tumemsajili Lameck Lawi kwa kufuata utaratibu. Wangesema kama ukichelewa kulipa mkataba unavunjika. Mpaka June tulikuwa tumemaliza kulipa pesa yote na nyaraka zote tunazo hata tukienda FIFA

“Kilichotokea Coastal Union wakapata deal kutoka nje ndio maana wakabadili maamuzi,” amesema Magori.

Acha ujumbe