Klabu ya Coastal Union ya Tanga imevunja mkataba na aliyekuwa kocha wao mkuu wa timu hiyo Yusuf Chipo kwa makubaliano ya pande zote mbili huku taarifa hiyo wakiitoa kupitia ukurasa wao wa Instagram.

 

Coastal Union Yavunja Mkataba na Kocha Wake

Coastal Union pia imemshukuru kocha huyo kwa mchango wake mkubwa na kipindi chote ambacho amewatumikia na anawatakia kila lakheri katika majukumu yake mapya huko atakapoenda.

Chipo hatakuwepo kwenye benchi lao la ufundi hii leo ambapo watakuwa wakiwakabili Yanga katika mchezo wao wa raundi ya 17 utakaopigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa majira ya saa 18:15.

Coastal Union Yavunja Mkataba na Kocha Wake

Coasta mpaka sasa baada ya michezo 16 waliyocheza wapo nafasi ya 13 na pointi zao 15 kileleni hadi sasa, wakiwa wameshinda michezo minne pekee na kupoteza michezo 9 sare zikiwa 3.

Leo hii wanahitaji ushindi ili waweze kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi kabla alam nyekundu ya kushuka daraja au kucheza play offs. Lakini je wataweza kutoka mbele ya Mabingwa watetezi?

Coastal Union Yavunja Mkataba na Kocha Wake

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa