Mshambuliaji wa Simba raia wa Serbia Dejan Georgjevic na Pape. O.Sakho ni miongoni mwa wachezaji 19 waliosafiri na timu kwenda nchini Sudan kwaajili ya michezo ya kirafiki itakayopigwa Agosti 28 na 31 mwaka huu.

Sakho, Dejan na Sakho Wamezungumza kabla ya Kuwafuata Asante Kotoko na Al Hilal, Meridianbet

Akiwa kwenye uwanja wa ndege wa Mwalim Nyerere Dejan alifanya mazungumzo na Mpenja TV na kuzungumzia juu ya uwepo wake Simba na mchango wake kama mshambualiji katika kufunga magoli zaidi ikiwa tayari ameshafunga goli moja kwenye ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar.

“Huu ndiyo Mwanzo tu, mashabiki wa Simba watafurahi, naamini cha Kwanza ni Timu kushinda lakini pia nitahakikisha wanasimba wanapata Furaha” Alisema Dejan.

Akigusia kuhusu msemo unaosambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii na mitaani wa “Mletee Mzungu” Dejan alisema kuwa anaufahamu na amekuwa akiusikia kutoka kwa marafiki na watu wengine wamekuwa wakimwambia Mzungu Mzungu”

Sakho, Dejan na Sakho Wamezungumza kabla ya Kuwafuata Asante Kotoko na Al Hilal, Meridianbet

Aidha, Pape Sakho amezungumza kuhusu Ubora wa Kikosi chao safari hii na namna wanavyokwenda kupata manufaa huko Sudan katika Michuano midogo iliyoandaliwa na Al Hilal.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa