Dickson Job Awaita Mashabiki kwa Mkapa

DICKSON Job beki wa Yanga ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Simba.

Novemba 5 2023 Uwanja wa Mkapa, Simba watakuwa wenyeji wa Yanga katika msako wa poiñti tatu muhimu.dickson jobDickson Job ambaye ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Miguel Gamondi amesema wanatambua umuhimu wa mchezo huo watapambana.

“Tuntambua umuhimu wa mchezo wetu ambao utakuwa mgumu hivyo tunawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kutushangilia na kutupa nguvu kwenye mchezo wetu.dickson job“Uwepo wao ni muhimu hasa ukizingatia wamekuwa pamoja nasi kwenye mechi nyingi ambazo tunacheza ni mwendelezo wao kuwa pamoja nasi tunaamini watatuongezea morali,”.

Dickson Job ni mchezaji wa kwanza kufunga ndani ya Yanga kwa msimu wa 2023/24 alipowafunga KMC mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Acha ujumbe