MABEKI wawili wa Klabu ya Yanga Dickson Job na Kibwana Shomari, wamefanikiwa kutimiza adhima yao ya kutaka kurejesha kidogo wanachokipata kwa jamii ya uhitaji mara baada ya kufanya zoezi hilo kwenye maeneo matatu tofauti.

Wachezaji ambao waliandaa mchezo wa hisani ambao uliopewa jina la Wape Tabasamu, uliwakutanisha mastaa mbalimbali wa Ligi Kuu Bara, uliochezwa kwenye Uwanja wa Sabasaba Morogoro na kiingilio chake kilienda kutimika kununua vitu mbalimbali.

Walitembelea Hodi ya Wazazi kwenye Hospitali ya Morogoro ambapo waligawa vitu mbalimbali kwa Watoto na kina mama waliotoka kujifungua hivi karibuni.

Baada ya hapo walikwenda kutembelea kituo cha kulelea Watoto Wenye Ulemavu wa akili na kuishi mazingira magumu cha Mehayo Center kilichipo Mazimbu Road. Kisha wakaenda kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Raya Islamic kilichopo Mzumbe mkoani Morogoro.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa