Dili la Feisal Kwenda Simba Limekufa

Inaelezwa kua kiungo wa klabu ya Azam Fc Feisal Salum hataweza kujiunga na klabu ya Simba tena baada ya klabu hiyo kuhamishia nguvu kwa mchezaji mwingine.

Klabu ya Simba inaelezwa ilikua na mpango mkakati wa kuhakikisha wanainasa saini ya kiungo Feisal kutoka Azam lakini dili hilo inasemekana kua limekufa kutokana na klabu ya Azam kutilia mkazo, Lakini pia klabu ya Simba kuelezwa kuhamishia nguvu kwa winga Elia Mpanzu.FeisalKlabu ya Simba ilikua ina mpango wa kumsajili kiungo huyo wa Azam baada ya kuondokewa na kiungo wake Clatous Chama ambaye ametimkia klabu ya Yanga, Lakini mpaka sasa inaelezwa dili hilo limekufa kwakua Azam Fc wameweka ugumu na Mnyama amehamishia mawindo wake upande mwingine.

Kwasasa klabu ya Simba kwasasa imeachana na mpango wa kumshusha Feisal Salum na kwasasa wakihamishia nguvu kwa mchezaji wa kimataifa wa Congo Elia Mpanzu anayekipiga klabu ya As Vita, Wekundu wa Msimbazi wanaamini mchezaji huyo anaweza kuja kuimarisha kikosi chao kwa kiwango kikubwa.

Acha ujumbe