Dilunga Aibukia Azam Fc

Kiungo wa zamani wa klabu ya Simba, Mtibwa Sugar Hassan Dilunga ameibukia ndani ya klabu ya Azam Fc baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na majeraha ambayo yamelimpata.

Kiungo Dilunga amekua nje ya uwanja kwa muda mrefu sana kutokana na kupata majeraha ya enka ambayo yalimfanya kutokuonekana uwanjani kwa kipindi kirefu pia, Lakini siku za karibuni kiungo huyo ameonekana katika kiwanja cha mazoezi cha klabu ya Azam akijifua.dilungaBaada ya kiungo huyo kuonekana ndani ya klabu ya Azam akijifua imeibua maswali mengi na wengi kujiuliza huenda mchezaji huyo atakwenda kujiunga na klabu ya Azam, Lakini mpaka wakati huu hakuna taarifa yeyote ambayo imetolewa na klabu ya Azam wala kwa upande wa mchezaji.

Kiungo Hassan Dilunga amekua nje ya uwanja tangu mwanzoni mwa msimu uliomalizika kutokana na majeraha yaliyompata kiungo huyo, Kiungo huyo kwasasa anaonekana kupona majeraha yake na kinachosubiriwa ni kumuona ataibukia ndani ya klabu gani kwa msimu ujao wa ligi kuu ya NBC.dilungaKlabu ya Simba haikumtaja Hassan Dilunga katika orodha ya wachezaji wake ambao wangeitumikia klabu hiyo kwa msimu huu wa 2022/23, Kitu ambacho kilionesha kua mchezaji huyo sio mali ya klabu ya Simba tena na ndio sababu ya kuhusishwa na klabu ya Azam kwa kipindi hichi ambacho anafanya mazoezi kwenye kiwanja cha klabu hiyo.

 

Acha ujumbe