Klabu ya Dodoma Jiji imepata ushindi wake wa 8 kwenye ligi hapo jana baada ya kumtwanga Polisi Tanzania mabao 2-1 kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Mchezo huo uliopigwa majira ya saa 2:30 usiku ulikuwa ukizikutanisha timu mbili ambazo zilikuwa zikihitaji pointi tatu muhimu kwaajili ya kujiweka salama kabla ya ligi kumalizika msimu huu.
Baada ya ushindi huo, Dodoma Jiji amepanda hadi nafasi ya 11 huku akiwa bado na kazi kubwa ya kufanya ili asalie ligi kuu, wakati kwa upande wa Maafande wao mambo yanazidi kuwaendea kombo.
Wapo nafasi ya mwisho kwenye ligi wakiwa na ushindi wa mechi nne pekee kati ya 25 alizocheza huku akikusanya pointi 19 tu hadi sasa huku mechi inayofuata atamenyana dhidi ya Singida Big Stars.
Baada ya ushindi huo, Walima Zabibu watacheza dhidi ya Coastal Union ya Tanga.