Dodoma:Serikali ya Tanzania imesema kuwa Ligi ya Muungano iliyokuwa inashirikisha timu kutoka Zanzibar na Timu zinachoza Ligi ya Tanzania bara itarudishwa hivi karibuni.

Dodoma:Ligi ya Muungano Kurudi Tena.

Akizungumza leo Septemba 13, 2022 Bungeni jijini Dodoma, Naibu Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Pauline Gekul alisema kuwa Wizara imekuwa kwenye mazungumzo na Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF), kuhakikisha kuwa Ligi hiyo inarudishwa.

“Mwanzoni ilisitishwa kwa sababu Zanzibar ilipata Uanachama wa CAF, wakawa wanapeleka timu zao mbili na huku upande wa bara (Tanzania) wanapeleka timu mbili, lakini kwa afya ya Muungano wetu, ila kitaifa tumekubaliana Ligi hii itarudishwa hivi karibuni na kamati imeshaundwa, tunaangalia tu tathmini ya gharama tu itakayotumika”. Naibu Waziri Pauline Gekul.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Azam Sports (@azamtvsports)

Aidha akigusia suala la utaratibu wa kuchagua wachezaji wa Timu ya Taifa Mhe, Gekul alisema kuwa Makocha hawakataliwi kuchagua wachezaji kutoka Zanzibar na Tanzania ili kunda Timu ya Taifa.

Dodoma:Ligi ya Muungano Kurudi Tena.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa