Straika wa Azam FC Prince Dube ametatua mjadala wa goli lilipi lilikuwa bora, kati ya lile alilowafunga Yanga msimu juzi kwa shuti kali kipa akiwa Mkenya Faruk Waza Shikalo na lile la juzi akimtungua kipa wa Simba Aishi Salumu Manula.

Dube amesema mabao yote hayo ni mazuri kuwahi kuyafunga yeye akiwa kwa Mkapa lakini kwa upande wake yeye kumfunga Manula ilikuwa ni wakati mzuri sana kwa na ndiyo bao lake bora kati ya hayo mawili.

Dube, Dube Alitaja Bao Lake Bora Kati ya Haya, Meridianbet

Dube alisema alipomfunga Shikalo na Yanga yake, goli lilikuwa wazi na alikuwa analiona vizuri, lakini wakati anamfunga Manula, ilikuwa ni kwenye upande mgumu ambao ilitakiwa utulivu ambao alikuwa nao kuweza kufunga.

“Mabao yote mazuri, kwa sababu niliwafunga makipa bora na timu bora na kubwa kuipa ushindi timu yangu. Lakini kwangu kumfunga Manula ilikuwa kitu bora sana.

 

“Ukitazama eneo ambalo nilikuwepo na namna ambavyo mpira niliupiga inakuwa siyo kitu rahisi lakini niliwezakufanikiwa na mpira ukazama wavuni,” alisema.

Dube alifunga bao dakika ya 35 kwenye mchezo wa ushindi kwa Azam wa bao 1-0 kwenye uwanja wa Mkapa na kuwafanya wavunje rekodi ya kutowafunga Simba kwa kipindi cha miaka mitano.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa