LEO Jumamosi Julai 9,2022 Yanga imeingia kwenye historia mpya ya kumpata rais ambaye ataiongoza timu hiyo kutoka kwenye mfumo wa kuongozwa na mwenyekiti, huku Eng Hersi akitamba kwenye uchaguzi huu.

Mpaka kufikia muda huu Yanga, Eng. Hersi Said aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM amechaguliwa kwa kura za ndio kwa asilimia 100 na kutangazwa kuwa rais mpya wa klabu hiyo.

Eng Hersi Yanga

Uchaguzi huo unafanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Dar.Mbali na kumchagua rais pia Yanga watachagua makamu wa rais pamoja na wajumbe watano.

Kwa upande wa wagombea nafasi ya umakamu kuna majina mawili ambayo ni Arafat Haji na Suma Mwaitenda. Ambao hadi kufikia muda huu ngoma imekuwa nzito kwenye kuamua nani anakwenda kuwa msaidizi wa Hersi.

Arafat alikuwa ni mtu wa karibu na Eng.Hersi kwenye kampeni za uchaguzi huo, huku Suma Mwaitenda ambaye ni mwanamke pekee, ambaye anaonekana kuwa jeshi la mtu mmoja.
Hadi kufikia jioni ya leo, Yanga watakuwa wameshawajua viongozi wao wapya ambao wataiongoza timu hiyo kwa muhula ujao ambao ni wa mabadiliko zaidi.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa