Farid Mussa: Chama Alinifanya Nisiende Simba.

KIUNGO wa Yanga SC Farid Mussa amefunguka na kueleza usajili wake ulivyokuwa, huku akimtaja mchezaji Clatous Chama kumfanya ashindwe kujiunga na Mnyama Simba ambaye kipindi hicho alikuwa wa moto sana. Beti na Meridianbet kwa ushindi mkubwa na machaguo kibao.

Farid Mussa amedumu Yanga kwa misimu yenye mafanikio zaidi kwake akiwa amefanikiwa kutwaa mataji matatu ya Ligi Kuu Bara, na mataji mawili ya ngao ya jamii huku akicheza hatua ya fainali Kombe la Shirikisho Afrika.

Farid Mussa amefunguka mambo mbalimbali huku akitaja mchezo wa fainali Kombe la Shirikisho Afrika;

“Hakuna tukio baya nimekutana nalo kama la msimu uliopita tukicheza mchezo wa fainali na kushindwa kutwaa taji kwa changamoto ya bao la nyumbani na ugenini mchezo wa kwanza tukiwa nyumbani dhidi ya USM Alger tulifungwa mabao 2-1 kwenye mchezo wa kwanza, kwani pamoja na sare ya jumla ya 2-2, lakini wamefaidika na mabao ya ugenini.”

Farid Mussa pia aligusia sakata lake la usajili katika klabu ya yanga, huku akiwa anahusishwa zaidi kujiunga na Simba. Meridianbet wanakupa nafasi ya kushinda Bodaboa mpya, TV, Simu Janja na zawadi kibao, ukibashri  mechi za EURO 2024.  PIGA BURE *149*10#

Kipindi hicho kikosi cha Mnyama Simba kilikuwa na mastaa kibao, na kupata namba ilikuwa ngumu sana, kutokana na uwepo wa wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa.

Moja kati ya wachezaji ambao walimpa wakati mgumu zaidi Farid Mussa kukubali kucheza Sima, ni Kiungo wa Zambia Clatous Chama kwani namba aliyokuwa anaimudu ni ile abayo Chama alikuwa wa moto sana.

Hiyo ndiyo ilimfanya Kiraka huyu kukubali kwenda Yanga, ili apate angalau uhakika wa kucheza, ikumbukwe malengo yake yalikuwa ni kurudi kucheza Hispania alipoondoka kutokana na janga la UVIKO 19.

Lakini hadi sasa bado yupo Yanga na anaendelea kuvaa medali, na kutwaa mataji ya ndani ya nchi. Cheza kasino na michezo  ya sloti, ushindi mkubwa upo kasino ya mtandaoni.

Acha ujumbe