Kocha mkuu wa Yanga mtunisia Nassredine Nabi amesema kuwa kuelekea katika ichuano ya kimataifa anahitaji kuona wachezaji wake wengi haswa katika eneo la kiungo wawe na uwezo mkubwa wa kuamua mechi hata kama washambuliaji wake watakuwa wamebanwa basi wao waweze kufunga mabao kama ambavyo Feisal Salum amekuwa akifanya.

Feisal Salum msimu huu amefanikiwa kuisaidaia Yanga kwa kufunga mabo nje ya boksi ikiwemo ktika mchezo wa nusu fainali ya kombe la Shirikisho dhidi ya Simba na katika fainali ya michuano hiyo dhidi ya Coastal Union.

Kocha huyo alisema katika michuano ya kimataifa ni ngumu sana kwa washambuliaji kufunga mabao ambapo mara nyingi hukosa nafasi za kufunga jambo ambalo linatakiwa kuamuliwa na viungo kwa kuhakikisha kuwa wanafunga mabao nje ya 18 au kutengeneza nafasi nyingi za kufunga kama ambavyo amekuwa akifanya Feisal Salum.

“Feisal napongeza ambacho amekuwa akifanya,amekuwa na uwezo  mzuri kwa sasa hivi ikiwa ni pamoja na kufunga nje ya boksi na hiyo ni njema haswa katika kuelekea msimu ujao ambao Yanga tutakwenda kushiriki michuano ya kimataifa ambapo mara nyingi washambuliaji huzuiwa na hukosa nafasi za kufunga.

“katika michuano ya kimataifa ukitazama mara nyingi timu ambazo zimefanikiwa ni kutokana kuwa na  aina ya wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao na kutengeneza zaidi nafasi,hivyo tutalifanyia kazi zaidi hilo ili tusiweze kuwa na msimu mbaya huko mbeleni”alisema kocha huyo.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa